Karibu

Mwaliko wa Baba Paroko

Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote. Asante kwa kutembelea tovuti yetu, karibu sana kusoma kwenye tovuti ya Kanisa Katoliki, Parokia ya Mwenyeheri Vincenza Maria Poloni - Ntyuka. Jimbo kuu la Dodoma

Ninayo furaha ya pekee kwa niaba ya wanaparokia wote wa Parokia ya Utatu Mtakatifu - Ntyuka, kukualika ndugu msomaji ushiriki na wanaparokia wa parokia yetu kuieneza Injili ya Yesu Kristu kupitia tovuti hii.

Baba Paroko

Matangazo, Habari & Matukio

Karibu usome matangazo, habari na matukio muhimu yanayohusu parokia yetu na jamii kwa ujumla.

Je, ungependa kushiriki katika uchangiaji kwa maendeleo ya parokia yetu?

shape
shape

Ijue Parokia

Historia ya Parokia

Historia ya Parokia ya Mwenyeheri Vincenza Maria Poloni ina asili yake iliyojengwa katika misingi ya Umoja, Upendo na Ushirikiano.

Parokia ya Mwenyeheri Vincenza Maria Poleni - Ntyuka ni zao kutoka Parokia ya Paulo wa Msalaba (Kanisa Kuu).

Parokia ya Mwenyeheri Vincenza Maria Poleni - Ntyuka ilitangazwa Parokia kamili na kuzinduliwa na Mhashamu Baba Askofu Mkuu Beatus Michael Kinyaiya, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma mnamo tarehe 12/12/2021.

Pamoja na Mhashamu Baba Askofu Mkuu, alikuwepo Makamo wa Askofu wa Jimbo Kuu la Dodoma Padri Onesmo Andrea Wiss na mapdre wengine.