![](https://ntyuka.tanzalight.co.tz/wp-content/uploads/2022/02/vyama.png)
Utume
Vyama vya kitume
Vyama vya kitume ni mhimili mkubwa katika kukuza, kuimarisha na kukoleza imani ya wakristo wakatoliki na utekelezaji wa shughuli za kitume/uinjilishaji hapa Parokiani.Wakristo wa Parokia ya Mwenyeheri Vincenza Maria Poloni walianza kumtumikia Mungu mapema kupitia vyama mbalimbali ya kitume tangu ngazi ya Kigango. Vyama vyote vya kitume vilivyoanzishwa vinaendelea kutekeleza majukumu yao hadi leo. Baadhi ya vyama vya Kitume vilivyo hai ni hivi vifuatavyo:
- Shirika la kipapa la Utoto Mtakatifu
- Lejio Maria (Moyo Safi wa Bikira Maria)
- WAWATA – Wanawake Wakatoliki Tanzania
- UWAKA – Umoja wa Wanaume Katoliki.
- Ushirika wa Moyo Mtakatifu wa Yesu.
- Ushirika wa Moyo Mtakatifu wa Yesu.
- VIWAWA - Vijana Wakatoliki Wafanyakazi
Viongozi wa vyama vyote wamechaguliwa kwa kuzingatia katiba ya Halmashauri ya Walei Taifa.