Malengo

Ijue Parokia

Malengo ya parokia

Kwa sasa viongozi wa Parokia ya Mwenyeheri Vincenza Maria Poloni wataendelea kuelekeza nguvu zao katika kuwahamasisha wakristo ambao kwa namna moja au nyingine kwa sasa hawajihusishi kushiriki shughuli za kanisa, kuwafuatilia kwa upendo wakristo wa parokia ambao wamelegalega na kuwasaidia waweze kumrudia Kristu. Kuhakikisha kuwa taratibu zote za uendeshaji wa shughuli za kitume hapa parokia  ya Utatu Mtakatifu Changanyikeni zinaboreshwa na zina msaidia Mkristu azidi kuimarika katika Imani yake asilegee kamwe, Kristu amkute angali anakesha (LK. 21:36; Mk 13:33; Ufu 6:17).

Parokia Inategemea kutekeleza shughuli mbalimbali katika mfumo wa mipango ya muda mfupi na muda mrefu kulingana na upatikanaji wa fedha na rasilimali mbalimbali za ujenzi wa Kanisa